Nuru Playground

Nuru ni lugha ya programu na mfumo wa kujifunzia ulioundwa mahsusi kwa ajili ya wazungumzaji wa Kiswahili. Lengo letu kuu ni kuwawezesha vijana kujifunza, kuunda, na kujaribu mambo mapya katika lugha wanayoizungumza nyumbani.